Sala Kwa Ajili ya Jumuiya ya Mwenye Heri Gérard


Bwana Yesu Kristu,

Kwa neema yako umeniita nikutumikie katika Shirika la Mwenyeheri Gerhard.

Nakushukuru kwa kunijalia neema hiyo.

Kwa maombezi ya Mama yetu Maria, Mtakatifu Yohane Mbaptizaji, Mwenyeheri Gerhard Tonque na watakatifu wote, kwa unyenyekevu naomba ili roho ya shirika letu ipenye maisha na matendo yangu ili niweze kujitoa kwa utumishi katika familia yangu, kati ya rafiki na yeyote mwenye kuhitaji msaada wangu.

Nikitumainia msaada wako, nataka daima niilinde imani na niwe na mapendo kwa jirani, hasa maskini, wenye huzuni, wapweke, vilema na wagonjwa.

 Nipe nguvu ninayohitaji kwa kuishi kadiri ya matakwa hayo kama Mkristu wa kweli anayejitolea nikitimiza maneneo ya Injili yako

 Kwa ajili ya utukufu ya Mungu, amani duniani na ustawi wa shirika letu.

 Amina


We thank Fr. Pius Mühlbacher O.S.B. and Br. Polykarp O.S.B. for this translation into Kisuaheli.


Bwana Yesu Kristo,

Kwa njia ya neema zako umeniita Mimi kukutumikia kama mwanajumuiya ya Mwenye Heri Gérard.

Ninakushukuru kwa kuniteua kwa wajibu huu.

Kwa maombezi ya Mama yetu, Mtakatifu Yohane Mbatizaji, Mwenye Heri Gérard Tonque na watakatifu wote, ninakuomba kwa unyenyekevu ili Maisha ya kiroho ya Jumuiya yetu yapenye Maisha na matendo yangu katika kujitoa kwa ajili ya utumishi wa familia yangu, marafiki zangu na yeyote anayehitaji msaada wangu.

Nikitegemea msaada wako, ninataka kila mara kulinda imani na kuwa na moyo ulio wazi kwa jirani hasa masikini, wenye huzuni, wapweke, wasiojiweza na wagonjwa.

Unijalie nguvu inayohitajika kuishi kama Mkristo muadilifu kulingana na roho ya Enjili na kulingana na uamuzi wangu.

Kwa ajili ya sifa na Utukufu wa Mungu, kwa ajili ya amani duniani na kwa faida ya jamii yetu.

Amina.


We thank Br. Markus Forster O.S.B. for this translation into Kisuaheli.Back to the homepage of the Brotherhood of Blessed Gérard


This page was last updated on Saturday, 16 April 2016 09:46:02